January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: miaka 60 ya uhuru, tulipofika si haba

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema  mafanikio yaliyofikiwa na Taifa katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru, si haba japo kilele cha matamanio ya Watanzania hakijafikiwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia amesema hayo leo Jumatano, tarehe 8 Desemba 2021, akihutubia Taifa kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika), yanayotarajiwa kufanyika  kesho alhamisi, katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

“Hatujafikia kilele cha matamanio yetu, lakini tulipofika si haba. Tutembee kifua mbele na kujisifu kwani mambo tuliyofikia kwa miaka 60 ni makubwa,” amesema Rais Samia.

Kiongozi huyo wa Tanzania ametaja baadhi ya mafanikio ambayo nchi imepata baada ya Tanzania Bara kupata uhuru wake kutoka kwa Waingereza, ikiwemo kulinda uhuru  na mipaka yake.

“Moja ya mafanikio ni kufanikiwa kuulinda uhuru wetu na mipaka yake, pili kujenga umoja wa kitaifa na mshikamano uliozaa na kulea utulivu na  amani tuliyo nayo, la tatu kuimarisha uchumi wetu na kupunguza umasiki kulikotuwezesha kutoka kwenye kundi la nchi masikini na kuingia katika kundi la nchi za uchumi  wa kati wa chini, la nne kuongeza na kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ametaja mafanikio mengine kuwa ni “la tano kujenga heshima ya nchi yetu na ushawishi kikanda na kimataifa, la sita ni kuimarisha demokrasia na utawala wa sheria.  Ndugu wananchi, inchi zote baadhi zilisambaratika na nyingine zilipoteza sehemu ya ardhi,  tunapoadhimisha miaka 60 ya uhuru  nchi yetu imebaki kuwa huru na mipaka yake kuwa salama.”

Rais Samia amesema, katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru, nchi imefanikiwa kuimarisha uchumi na kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kati wa chini, kabla ya 2025, ilivyokadiriwa katika Dira ya Taifa.

“Katika kipindi cha miaka 60 tumefanikiwa kujenga nchi yetu au uchumi  wetu hadi kufikia nchi au  uchumi wa kati wa chini mapena zaidi  kabisa kuliko tulivyokadiria kwenye malengo ya  dira ya taifa ya kufikia hadhi hiyo ya mwaka 2025. Wastani wa pato kwa mtu kwa mwaka 1961 ilikuwa Sh.  776 na mwaka jana ilikuwa ni Sh.  2,653,790,  jambo hili linaongeza hadhi yetu machoni mwa jumuiya za kimataifa na kutuondolea unyonge na unyanyapaa,” amesema Rais Samia.

Mafanikio mengine yaliyotajwa na Rais Samia, ni uboreshwaji wa miundombinu ya usafirishaji wa ardhini, angani, majini na reli.

“Tumeweza kuiunganisha nchi yetu kwa miundombinu ya usafiri na usafirishaji kwa kujenga mitandao ya barabara, kuimarisha usafiri wa anga, majini na usafiri na usafiri wa reli. Tofauti na 1961,  leo unaweza fika pembe yoyote ya Tanzania ndani ya saa 24 wakati tunapata uhuru wakoloni walituachia km za lami zisizodizi 1,360 na sasa mtandao wa barabara za lami umefikia refu wa km11,186 na kazi inaendelea,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema nchi inaendelea kuunganisha makao makui ya mikoa kwa barabara zenye kiwango cha lami “ikumbuwke kuwa,  hapa tunazungumzia nchi yenye ukubwa wa kilomita za mraba 950,000,  mtandao tulioujenga ungeweza tosha na mtandao wa baraba za nchi nyingine,”

Amesema Serikali inaendelea kuimarisha usafiri wa anga kwa kuboresha utendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), ambapo imefanya malipo ya awali ya ununuzi wa ndege tano.

“Kutokana na kukuwa kwa shughuli za uchumi kwa sasa  uzafiri wa anga si suala la anasa au starehe, kufufuliwa au kuimarishwa ATCL ni jambo la lazima. Kwa sasa lina jumla ya nsege 12 na tayari tumefanya malipo ya awali ya ununuzi wa  ndege nyingine tano. Sasa ATCL lina ndege tumeza kuliwezesha shirika kufanya safari za ndani na nje ya nchi,” amesema Rais Samia.

Pia, Rais Samia ameelezea mafanikio katika usafiri wa majini na reli, akisema “kwa upande wa usafiri wa majini jitihada zimefanyika,  bahari na maziwa zitumike kama njia bora na salama za usafiri na usafirishaji,  kabla ya uhuru tulikuwa na meli sita  na sasa tuna meli 14.  Tulikuwa na vivuko vitatu na sasa tuna 33.”

“Wakati tunapata uhuru nchi yetu ilikuwa na njia sita za mtandao wa reli uliokuwa na urefu wa km 2,405 na baada ya uhuru tumeongeza njia mbili ya Ruvu Mluazi na Manyoni Singida, ambazo umefanya mtandao kufikia km 2,707,” amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!