RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Maridhiano day yatakayofanyika tarehe 3 Machi mwaka huu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari jana tarehe 28 Februari, 2022 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhaji Mussa Salumu ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema jumuiya hiyo inatimiza miaka 6.
Amesema Jumuiya hiyo ilisajiliwa rasmi tarehe 3 Machi, 2016 lengo likiwa ni kushirikiana na serikali kuhimiza amani na utulivu kwa watanzania wote.
Amesema Jumuiya ya maridhiano Tanzania ni jumuiya inayoudwa na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali hapa nchini Tanzania bila kujali itikadi ya chama wala dini yoyote.
“Malengo ya Jumuiya ya maridhiano ni kuleta mwafaka katika mambo yanayosababisha tofauti katika dini, mila, siasa na madhehebu mbalimbali ya dini.
“Kusaidia juhudi za serikali katika jitihada zake za kuondoa au kupunguza umasikini, kama ile ya wakulima na wafugaji,” amesema Mwenyekiti.
Aidha, amesema katika maadhimisho ya wiki ya maridhiano day wamekuwa wakichangia damu takribani nchi nzima kwa lengo la kuwasaidia watu wenye uhitaji.
“Hii ni siku ya ambayo wana maridhiano wa nchi nzima tumekubaliana kuiadhimisha kwa uchangiaji wa damu ili kuokoa maisha ili kuokoa maisha ya mama na mtoto, watu waliopata ajali na wagonjwa mbalimbali.
“Hili ni zoezi ambalo litahitimishwa siku ya tarehe 03 Machi 2022 kwa shughuli maalum katika ukumbi wa itakayofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Concentration Centre hapa mjini Dodoma, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa saba 7 mchana” amesema Mwenyekiti.
Leave a comment