RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana kwa mara nyingine na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Chadema, Freeman Mbowe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Wawili hao wamekutana leo Jumatatu tarehe 9 Mei 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Hii ni mara ya pili wanakutana na kuzungumza masuala mbalimbali yenye tija kwa Taifa.
Mara ya kwanza ilikuwa tarehe 4 Machi 2022, saa chache tu kupita tangu Mbowe alipoachiwa huru na Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi katika kesi ya ugadia aliyokuwa anakabiliwa nayo pamoja na wenzake watatu.
Katika mazungumzo hayo ya 4 Machi 2022, Rais Samia na Mbowe waliueleza umma wamekubaliana kushirikiana na kutangaza haki kwa mustakabali mpana wa Taifa.
Katika mazungumzo ya leo Jumatatu haijafahamika zalichozungumza.
Leave a comment