July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Machinga tuendelee kuvumiliana

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa wafanya biashara wadogo wadogo ‘machinga’ kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kwa kuwa kazi ya kuwaondoa barabarani ni kwa nia njema ya maendeleo yao wenyewe hapo baadae. Anaripoti Matilda Buguye… (endelea)

Pia amesema uamuzi wa Serikali unalenga kuwajengea mazingira na sasa inaendelea kukusanya fedha kwa ajili ya kuwajengea maeneo mazuri na yakudumu kwa ajili ya biashara zao. 

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Disemba, 2021 katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka awamu ya pili, Mbagala rangi tatu jijini Dar es salaam.

Huku akiambatana na viongozi mbalimbali wa serikali katika hafla hiyo iliyopambwa na vikundi mbalimbali vya burudani ilivyoshuhudiwa na wananchi wa Mbagala walioweza kuhudhuria kwenye hafla hiyo.

Aidha, Rais Samia awakemea baadhi ya wananchi wasiokua na uzalendo ambao wanajihusisha na kuhujumu jitihada za utekelezaji wa mradi  huo wa ujenzi kwa kufanya vitendo vya wizi wa vifaa mbalimbali vinavyotumika.

Hivyo awaomba wananchi walio na uzalendo watakapogundua juu ya uhujumu wa aina yeyote juu ya ujenzi huo waseme na kutoa taarifa sehemu husika.

error: Content is protected !!