RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kwenda nchini Kenya kwa ajili ya ziara ya siku mbili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Kwa mujibu wa Kanze Mararo, Msemaji wa Ikulu nchini Kenya, ziara hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 4 Mei 2021 ambapo Rais Samia atafanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta wa taifa hilo
Alipoulizwa na chombo kimoja cha habari nchini kuhusu safari hiyo, Gerson Msigwa ambaye ni Msemaji wa Ikuli ya Tanzania, amesema Wizara ya Mambo ya Nje ndio wenye jukumu hilo.
Emmanuel Buhohela, Ofisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje, amesema waziri atalizungumzia hilo.

Tarehe 22 Machi 2021, akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya taifa lake jijini Dodoma, wakati wa kuaga mwili wa Hayati John Magufuli, Rais Kenyatta alimkaribisha Rais Samia nchini kwake.
Hata hivyo, tarehe 10 Aprili 2021, Kenyatta alituma ujumbe maalumu nchini ulioongozwa na Waziri wa Michezo, Utamaduni na Urithi wa nchi hiyo, Balozi Amina Mohamed.
Leave a comment