
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, yupo Maputo nchini Msumbiji kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Mkutano huo, utafanyika leo Jumatano tarehe 23 Juni, 2021.
Mkutano huo unafanyika mjini Maputo Msumbiji ambapo Rais Filipe Nyusi ndio Mwenyekiti wa sasa wa SADC.
Rais Samia aliondoa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma kwenda Msumbiji jana jioni, tarehe 22 Juni 2021.
Uwanjani hapo, Rais Samia aliagana na viongozi mbalimbali akiwemo, Dk. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Tanzania.
More Stories
DUWASA wakata maji Soko la Mavunde, wafanyabiashara walia
Mkurugenzi Mkuu UNESCO Duniani atoa ujumbe siku ya Kiswahili duniani
Simbachawene kuongoza harambee kampeni GGM Kili Challenge 2022