May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia kushiriki mkutano SADC Malawi

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Jumatatu tarehe 16 Agosti 2021, anaondoka jijini Dodoma kwenda nchini Malawi kushiriki mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema, mkutano huo utaanza kesho Jumanne tarehe 17 na 18 Agosti 2021.

Katika Mkutano huo wa 41 pamoja na mambo mengine, Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC, watathibitisha nchi ya Malawi kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja (Agosti 2021 – Agosti 2022).

error: Content is protected !!