RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema, atafanya mabadiliko ya makatibu wakuu wa wizara mbalimbali hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Amedokeza hilo leo Alhamisi tarehe 1 Aprili 2021, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, mara baada ya kumaliza kuwaapisha mawaziri, naibu mawaziri na katibu mkuu kiongozi waliowateua jana Jumatano.
Akianza kuzungumza kwa kuwasalimia viongozi mbalimbali waliohudhulia hafla hiyo, Rais Samia aliuliza makatibu wakuu mpo, heloooo…kisha wakasimama kumsalimia naye akasema mmetulia ninyi “siyo leo lakini nakuja.”
Mara baada ya kumaliza hotuba yake fupi, Rais Samia akizungumzia sikukuu ya Pasaka akisema kuanzia kesho Ijumaa hadi Jumatatu ni sikuu “tutakutana hapa Jumanne” kushuhudia wengine wakiapishwa.
Hata hivyo, Rais Samia hakusema hasa hiyo Jumanne, watakaoapishwa watakuwa makatibu wakuu au wengine, kama wakuu wa mikoa, wilaya au makatibu tawala wa mikoa.
Rais Samia amewaonya wateule wake, watakaokuwa wakipandisha mabega akisema “nitakuwa na kipimo cha mabega, nikiona mtu anapandisha mabega nitaona huyu si mtumishi wa wananchi.”
Leave a comment