August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia kufuata nyayo za Mkapa ushirikishaji sekta binafsi

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameitaka jamii ibadili mtizamo wa kwamba Serikali inaweza kufanya kila kitu peke yake, bila ya ushirikishwaji wa sekta binafsi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Wito huo umetolewa na Rais Samia, leo Alhamisi tarehe 14 Julai, 2022, akizungumza katika kongamano la pili la kumuenzi Rais Mstaafu wa Tanzania, Hayati Benjamin Mkapa, lililofanyika visiwani Zanzibar.

Mkuu huyo wa nchi amesema, kama nchi inataka kwenda kwa kasi katika kufikia maendeleo hususan katika sekta ya afya, inabidi sekta binafsi ishirikishwe katika mipango ya maendeleo.

“Ikiwa tunataka kwenda kwa kasi na kufikia malengo yetu ya 2030 ya kuwa na afya kwa wote, basi hatuna budi kubadili mtizamo wetu kuwa tunaweza kufanya hilo peke yetu, zile enzi za kwamba Serikali itafanya yenyewe kila kitu nadhani tunabidi tubadilike, lazima tushirikishe sekta binafsi ili twende kwa kasi na kupata matokeo tunayotaka,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amewataka watendaji wa sekta ya afya kushirikisha sekta binafsi katika kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi wa afya.

“Wito wangu kwa wanaosimamia masuala ya rasilimali watu katika sekta ya afya kutoa kipaumbele zaidi katika kuharakisha utekelezaji mikakati ambayo tayari imeshabainishwa kutatua changamoto ya watumishi. Shirikianeni na asasi za kiraia muendelee kuimarisha eneo hili kwa nia ya kufikia malengo ya kitaifa na kimataifa ifikapo 2030,” amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!