RAIS wa Tanzania, Samia Sulkuhu Hssan amempongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Jenister Mhagama kwa kuweza kumudu kila wizara anayopangiwa kuhudumu huku akimtaja kuwa ni “jembe” na “kiraka”. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).
“Nimshukuru sana Waziri Jenista, jembe. Unajua Jenista ni kiraka, ukikiweka kwa vijana utafikiri amekaa nao miaka 100, ukimpeleka bungeni huko ndio anacheza lakini tumempeleka utumishi unawajua utafikiri amekaa na hii wizara miaka 50,” amesema.
Mkuu huyo wa nchi ametoa pongezi hizo kwa Waziri wake leo Jumapili tarehe 27, Novemba 2022, wakati akifungua mkutano mkuu wa 10 wa chama cha Taaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) unaofanyika jijini Arusha.
Rais Samia amemshukuru Jenista na timu yake yote kwa kusimamia kwa kusimamia uzingatiaji wa taalua mbalimbali katika utumishi wa umma ikiwemo watunza kumbukumbu na kuhakiisha changamoto zao zinatatuliwa mara kwa mara zinapotokea.
Leave a comment