Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Rais Samia: Hivi nina maradhi gani na katiba mpya
HabariTangulizi

Rais Samia: Hivi nina maradhi gani na katiba mpya

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amejishangaa jinsi ambavyo amekuwa akilitaja jina la Bunge la Katiba, badala ya Bunge la Bajeti. Anaripoti Mwandishi Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Ni baada ya jana Jumatano na leo Alhamisi tarehe 1 Aprili 2021, kulitaja Bunge hilo ambalo yeye alikuwa makamu wake mwenyekiti huku Hayati Samuel Sitta, akiwa mwenyekiti.

Jana Jumatano, katika mazungumzo yake kwenye hafla ya uapisho wa Dk. Philip Mpango, kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, alijikuta alitaja jina la “Bunge la Katiba” badala ya Bunge la Bajeti ambalo limeanza vikao vyake jijini Dodoma.

Leo Alhamisi, Rais Samia baada ya kumaliza kuwaapisha mawaziri, naibu mawaziri na Balozi Hussein Kattanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, amejikuta tena badala ya kusema Bunge la Bajeti, linaloendelea na vikao vyake, akataja Bunge la Katiba.

“Hivi nina maradhi gani na katiba, nafikiri wamenipushi pushi sana kuhusu katiba katiba lakini wasahau kidogo,” amesema Rais Samia huku wageni waliohudhulia hafla hiyo wakifurahia

Prof. Palamaganda Kabudi, Waziri wa katiba na Sheria

Tangu alipoingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, alipoapishwa kuwa Rais wa Tanzania baada ya aliyekuwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.

Dk. Magufuli, alifikwa mauti tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa ugonjwa wa mfumo wa umeme wa moyo na mwili wake, kuzikwa nyumbani kwao, Chato mkoani Geita.

Baada ya Rais Samia kuingia madarakani, kumekuwa na kauli kutoka makundi mbalimbali wakimwomba auendeleze mchakato wa Katiba mpya hasa ikizingatiwa yeye alikuwa miongoni mwa waliosimamia kupatikana kwa Katiba inayopendekezwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Bunge lalia msongamano wa mizigo bandari Dar es Salaam

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

error: Content is protected !!