January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia azungumzia janga la UVIKO-19, chanjo

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasihi wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya virusi vya korona (UVIKO-19) na kujitokeza kupata chanjo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Katika hotuba yake kuufunga mwaka waka 2021, aliyoitoa leo Ijumaa tarehe 31 Desemba 2021 na kurushwa na vyombo vya habari, Rais Samia amesema, dunia bado inakabiliwa na UVIKO – 19 na kwa sasa tupo katika wimbi la nne la ugonjwa huo.


Amesema, kirusi kipya cha Omicron kinaenea kwa kasi kubwa, na tayari kipo na kimeshaingia nchini kwetu.

“Niwakumbushe kuchukua tahadhari kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa afya,” amesema

Rais Samia amesema, “nitumie fursa hii kuwahimiza wananchi kupata chanjo dhidi ya UVIKO – 19.”

“Natambua kuwa chanjo haizuii mtu kupata maambukizi, ila inapunguza makali ya ugonjwa huo. Hivyo niwahimize wananchi kwenda kuchanja. Chanjo zipo na zinapatikana bila malipo,” amesisitiza

Rais Samia amesema, mwaka 2021, tuliendelea kukabiliana na janga la UVIKO – 19, ambalo linaendelea kuisumbua dunia hadi hii leo.

“ Janga hili lilisababisha kuzorota kwa kasi ya ukuaji wa uchumi, kutoka ukuaji wa asilimia 7 mwaka 2019/2020 hadi asilimia 4.8 mwaka 2020/2021,” amesema

error: Content is protected !!