Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia awatolea uvivu vijana kuhusu ajira
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia awatolea uvivu vijana kuhusu ajira

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, amewataka vijana watumie mazingira mazuri ya kibiashara na uwekezaji yaliyopo nchini kujiajiri kwa kuwa Serikali kazi yake siyo ya kutengeneza ajira. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametoa ushauri huo leo Jumanne, tarehe 10 Januari 2023, akifunga matembezi ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), visiwani Zanzibar.

“Nilikuwa naangalia jana au juzi kwenye Tv, Watanzania wanahojiwa kuhusu ajira kwa hiyo kila anayehojiwa anamalizia Serikali itenge ajira. Nataka kuwambia kazi ya Serikali si kutengeneza ajira, ni kuweka mazingira mazuri ili muyatumie kutengeneza ajira na hiyo kazi tunaifanya vya kutosha. Naomba muende mkatengeneze ajira kwa mazingira yaliyokuwwepo,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amewataka vijana kutumia fursa zilizopo katika uchumi wa buluu kujiajiri na kuongeza kipato, huku akiwaonya kukwepa tabia ya kupenda utajiri wa harakahara.

“Vijana wa leo tunakimbilia kwenye kuutaka utajiri uwe na jumba zuri na gazi zuri, lakini baada ya muda utajiri unakugeuka unakupiga mambo yote huwezi kuyatunza unarudi kwenye unyonge.Utajiri ulioutaka kwa harakaharaka unakupiga. Tunatakiwa kutengeneza ukwasi wa kila wakati, upatikanaji wa fedha kila wakati, muwe na miradi midogo midogo,” amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amewataka vijana wawe wabunifu katika kuanzisha biashara mpya, huku akiwaasa wajikite katika kilimo cha mazao ya biashara na chakula.

“Kilimo ni sehemu nyingine mnaweza mkafanya kazi vizuri kabisa, tunakokwenda huko kuna tatizo la upungufu wa chakula tunaweza tukazalisha mboga na chakula kwa wingi sana tukajitosheleza na tukauza kwa wengine. Nawaomba vijana kajengeni uchumi wa nchi, mtusaidie Serikali zile tunazokusanya juu ziende kwenye miradi ya maendeleo,” amesema Rais Samia.

Pia, Rais Samia amewataka vijana kuandaa mawazo mazuri ya biashara ili waweze kupata mikopo ya masharti nafuu inayotolewa na taasisi za Serikali.

Rais Samia amesema kazi ya Serikali ni kufanya makusanyo makubwa na kufanya miradi itakayoleta mzunguko wa fedha kwa ajili ya kuwawezesha vijana kujiairi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

error: Content is protected !!