May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia awatakia kheri watahiniwa kidato cha sita

Wanafunzi wa kidato cha sita walipokuwa wanafanya mtihani

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan amewatakia wanafunzi wote wa kidato cha sita kila kheri,katika mitihani yao iliyoanza leo jumatatu tarehe 9 mei 2022 , Pamoja na Walimu Tarajali wanaosomea ualimu ,wanaoanza mitihani yao leo. Anaripoti Rhoda Kanuti, Dar es Salaam … (endelea)

Katika ukurasa wake wa Twitter ,Rais Samia leo jumatatu ameandika ‘’nawatakia kila kheri wanafunzi wote wa kidato cha sita , pamoja na walimu tarajali wanao somea ualimu.’’

Aidha Samia amesema serikali itaendelea kuhakikisha inaongeza nafasi na mazingira bora, kwenu katika kufanikisha muweze kusonga mbele kielimu ,kiajira ili nchi iwenze kunufaika na ujenzi wa vipaji vyenu.
Jumla ya watahiniwa 95,955 kutoka shule za sekondari 841 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 250 wameanza mitihani ya kumaliza kidato ya sita leo.

Pia watahiniwa 9,670 kutoka vyuo 70 wamesajiliwa kufanya mitihani ya mwisho ya kozi ya ualimu katika ngazi ya stashahada na cheti.

error: Content is protected !!