December 4, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia awatakia heri watahiniwa darasa la saba

Wanafunzi wa darasa la saba wakifanya mtihani

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewatakia heri watahiniwa wanaofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi, huku akiwaahidi kwamba Serikali itahakikisha inaandaa mazingira mazuri ya kujiunga na elimu ya sekondari 2023. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametoa ujumbe huo leo Jumatano, tarehe 5 Oktoba 2022, ikiwa wanafunzi hao wa darasa la saba, wanaanza kufanya mitihani hiyo ya siku mbili, iliyoanza leo hadi kesho Alhamisi, tarehe 6 Oktoba mwaka huu.

“Nawatakia kila la kheri wanangu wote mnaoanza mtihani wa darasa la saba leo. Mwenyezi Mungu awape utulivu na siha njema ili mfanye vizuri mitihani yenu. Serikali itahakikisha maandalizi ya miundombinu ya kuwapokea wote watakaoendelea na kidato cha kwanza mwakani 2023 inakamilika,” ameandika Rais Samia kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana tarehe 4 Oktoba 2022 na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Athuman Amasi, jumla ya watahiniwa 1,384,340 wanatarajia kufanya mtihani huo.

error: Content is protected !!