July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia awasili Burundi

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekwisha kuwasili nchini Burundi kuanzia ziara ya siku mbili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Rais Samia aliagana na viongozi mbalimbali, waliojitokeza kumsindikiza.

Katika Uwanja wa Kimataifa Melchion Ndadaye jijini Bujumbura Burudi, Rais Samia amepokelewa na Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza.

Rais Samia amefanya ziara hiyo ya Kitaifa ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye.

Mara baada ya kuwasili, alikwenda Ikulu ya Burundi ambapo alipata fursa ya kuzungumza na mwenyeji wake, Rais Ndayishimiye na baadaye zilipigwa nyimbo za mataifa hayo na mizinga 21 kupigwa.

Rais Samia amekagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake.

Akiwa nchini humo, atashuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari.

Aidha, Rais Samia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la Wafanyabishara wa Burundi na Tanzania kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na Burundi.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!