Sunday , 26 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia awapa ujumbe majaji ‘katendeni haki
Habari za Siasa

Rais Samia awapa ujumbe majaji ‘katendeni haki

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka Majaji saba wa Mahakama ya Rufaa na 21 ya Mahakama Kuu ya Tanzania, kwenda kutenda haki. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa wito huo leo Jumatatu tarehe 17 Mei 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kuwaapisha majaji saba wa Mahakama ya Rufani na 21 wa Mahakama Kuu, aliowateua 11 Mei 2021.

Amewaonya majaji hao kuwa, kama watakwenda kinyume na viapo vyao, watakuwa wamepoteza sifa za kuendelea kushika wadhifa huo.

“Nawaombeni mkaongoze vyema lakini mkaongozwe vyema na nafsi zenu na hili nalirudia, kwamba katika utendaji haki, kanuni na sheria zinazotungwa na Bunge kuja kwenu asilimia 70 ni kazi yenu na asilimia 30 ikaongozwe na utu na nafsi zenu,” amesema Rais Samia.

Amesema “nafsi zenu ikiwaelekeza kuchukua pesa na kunyima haki za wengine, ujue umetetereka na tukikugundua utakua umekosa sifa zilizokufikisha hapa.”

Rais Samia amewaeleza majaji hao kuwa, majukumu yao ni kutenda haki kwa Watanzania, kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Tambueni jukumu lililo mbele yenu ni kubwa sana, Katiba yetu inatamka kuwa mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mahakama, hili ni jukumu zito na kubwa sana sana katika kutenda haki,” amesema Rais Samia.

Biswalo Mganga (kulia) akiapa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan

Amewaagiza majaji hao wakatatue changamoto ya mlundikano wa mashauri.

“Na leo ni imani yangu baada ya uteuzi huu, tatizo hili litatapungua kufuatia uteuzi huu uliofanywa. Idadi ya majaji ya Mahakama Rufaa imeongezeka kutoka 17 wa awali kufikia 24, na wa Mahakama Kuu kutoka 71 hadi 86.”

“Najua idadi haitoshi lakini ongezeko la leo si haba, naimani kasi ya uendeshaji kesi itaongezeka,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ameagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), kuharakisha upelelezi.

“Naagiza vyombo ya upelelezi ofisi ya DPP, Polisi na Takukuru kuharakisha kesi, wakati mwingine kesi hazicheleweshwi na mahakama bali upelelzi,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!