January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia awaonya UVCCM “acheni kudhalilishana”

Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

MWENYEKITI wa chama tawala nchini Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amewaonya vijana wa chama hicho, kuacha kudhalilishana wakati wa uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pemba … (endelea).

Aidha, amewataka kutokubali kutumika na wanaotafuta uongozi kwani kufanya hivyo hakuna tija kwao na ama ndani ya chama hicho.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, tarehe 7 Januari 2022, katika kilele cha matembezi ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yaliyofanyika wilaya ya mkoani Kusini Pemba na kuratibiwa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Amesema, mwaka huu kunafanyika uchaguzi wa ndani wa chama hicho hivyo wale wote watakaokwenda kinyume na sheria na kanuni za chama hicho wataenguliwa.

“Uzoefu unaonesha vijana mnageuzwa ngazi sana, mnadanganywa na vifedha vidogo na tamaa za nafasi, mnainamishwa migogo na watu wanapanda juu ya migogo yenu, wakishapata wanachokitaka wanawaacha. Kama wote mnaowabeba wangefanyiakazi haki zenu, changamoto nyingi zenu zisingekuwepo,” amesema Rais Samia.

“Niwaombe chaguzi zetu za jumuia za Chama Cha Mapinduzi, zinasimamiwa na kanuni na miongozo, vijana mna haki zote za kuchagua na kuchaguliwa, nendeni kagombeeni na mimi nawahakikishia, zitakapokuja juu kwetu tutatizama sura, tutatizama uwezo, weledi na umakini wa mtu katika kufanya kazi zake,” amesema.

Mwenyekiti huyo wa CCM amewasihi vijana hao akisema, “nendani kasimameni kwa miguu yenu.”

Pia, ametumia fursa hiyo kuwaonya vijana hao kuacha fitna na kuchongeana hususan kwa wasichana kwani kuna nyakati anaweza kupokea simu 100 za malalamiko au kufitiniana.

“Katika chaguzi zenu kunatawala fitina, rushwa na mambo kadhaa. Ukifika uchaguzi wa vijana sisi wenye vijana wa kike mioyo inadunda, mwanamke ni kijana, wote wana haki sawa, achene kudhalilisha dada zenu, anayesimama mwenye sifa apewe nafasi, yale mliyoyazoea yaacheni,” amesema

error: Content is protected !!