RAIS Samia Suluhu Hassan amewaomba wananchi wa mkoa huo kupunguza matayarisho ya kinywaji maarufu mkoani humo cha pombe aina ya mbege, ili kupunguza matumizi ya nafaka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumamosi tarehe 22 Januari, 2022 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) wakati akizindua Tamasha la utamaduni mkoa Kilimanjaro, ambalo pia alikuwa mgeni rasmi.
Akitubia wananchi na wageni mbalimbali waliohudhuria tamasha hilo, Rais Samia ambaye pia ni Chifu Hangaya amesema mwaka huu kutakuwa na upungufu wa chakula kidogo.
“Pamoja na kwamba hatukuweza kupanda
mwezi Oktoba lakini tuna akiba ya kutosha ya chakula, niwaombe sana ndugu zangu Kilimanjaro tupunguze kidogo matayarisho ya mbege na vinywaji vingine kwa kutumia nafaka zetu.
“Tujue kwamba mwezi wa 10 hatukupanda, tutapanda mwezi Machi na kutakuwa na upungufu kidogo wa chakula, tutumie chakula tulichonacho ili kije kitufae huko mbele,” amesema Rais Samia.
Aidha, amewaomba Watanzania kuendelea kuomba kwa imani zetu mbalimbali ili Mwenyezi Mungu ajalie mvua yenye neema na baraka.
“Iiendelee kunyesha na kumaliza tatizo la ukame linaloendelea na kuteketeza mifugo na kutuzuia kwenda kwenye kilimo nami Chifu Mkuu nitaendelea kuwa pamoja nanyi katika maombi hayo.
Leave a comment