August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia awamwagia pongezi Serengeti Girls

Rais Samia Suluhu Hassan akishuhudia mchezo kati ya Simba Na Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameipongeza Timu ya Taifa hilo ya soka la Wanawake chini ya miaka 17 ‘Serengeti Girls’ kwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia nchini India Oktoba 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Serengeti Girls walifuza jana Jumapili tarehe 6 Juni 2022 baada ya kuwaondoa Caremoon katika michezo miwili iliyopigwa.

Mchezo wa awali uliopigwa Cameroon, Sereengeti Girls iliibuka na ushindi wa 4-1 na ule uliipigwa jana Uwanja wa Aman Zanzibar ikaibuka na ushindi wa 1-0 hivyo kufuza kwa jumla ya magoli 5-1.

Hii ni mara ya kwanza Serengeti Girls inafuzu michuano hiyo mikubwa duniani.

Mara baada ya kufuzu, Rais wa Tanzania, Samia alitumia ukurasa wake wa Twitter kuwapongeza akisema, “nawapa Pongezi Timu ya Taifa ya Soka la Wanawake chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2022.”

“Hongera kwa benchi la ufundi na wote waliochangia kufikia hatua hii. Mmeweka historia kubwa na adhimu kwa nchi yetu. Ninyi ni fahari ya Watanzania.”

error: Content is protected !!