August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia awaibua Chegeni, Serukamba, Chalamila, Hapi atupwa nje

Albert Chalamila

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan, amewateuwa Raphael Chegeni, aliyekuwa Mbunge wa Busega na Peter Serukamba, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, kwenye wadhifa wa ukuu wa mkoa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Chengeni amepangiwa kufanya kazi yake, mkoani Mara, huku Serukamba akipelekwa mkoani Singida.

Naye mwanasiasa mtata, Albert Chalamila, ambaye amewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na Mwanza na baadaye kuondolewa kwenye wadhifa huo, amefanywa kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera.

Ally Hapi

Aidha, katika mabadiliko hayo, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara, Ally Salum Hapi, ametupwa nje ya uongozi.

Hapi ni miongoni mwa watumishi wa umma, waliokuwa wakitajwa katika tuhuma mbalimbali za ukosefu wa maadili na wanaokwenda kinyume na utawala bora.

Mbali na Hapi, wanasiasa wengine mashuhuri waliotupwa kwenye uteuzi huo mpya, ni David Kafulila, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu na Stephen Kagaigai, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro. Kagaigai aliwahi kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Orodha kamili ya wakuu wa mikoa wapya na vitu vyao vya kazi ni kama ifuatavyo:

error: Content is protected !!