August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia awafuta machozi wanafunzi wenye mahitaji maalumu Songea

Spread the love

JUMLA ya wanafunzi 16 wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi Subira iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa bweni katika shule yao. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake hivi karibuni, Stanslaus Dominic amesema wanafunzi wengi walishindwa kuhudhuria masomo kutokana na umbali pamoja na gharama za kufika shuleni hapo.

Amesema kutokana na ujenzi wa bweni hilo, sasa wanafunzi watafika wengi shuleni hapo kupata elimu na kusoma kwa bidii.

 

“Tunamshukuru Rais wetu Samia Hassan Suluhu kwa kutujengea mabweni ili tusome vizuri. Tulikuwa tunatembea umbali mrefu lakini sasa naahidi kusoma kwa bidii,” amesema.

Aidha, Mwalimu Mkuu, Kanisi Sindunguru amesema awali wakati hapakuwepo na bweni, mahudhurio darasani kwa wanafunzi hao yalikuwa ya kusuasua lakini sasa baada bweni hilo kukamilika ari ya masomo imeongezeka.

Naye Diwani wa Kata ya Subira, John Ngonyani (CCM) amesema katika kata hiyo peke yake kuna watoto wengi wenye mahitaji maalumu.

“Hapa kuna watoto 16 ila waliopo mtaani ni wengi na wote wanashindwa kuja shule kutokana na mazingira waliyopo.

“Ila kutokana ujenzi wa bweni hili nina imani watoto wote waliopo mtaani sasa watakuja kupata elimu hii vizuri zaidi kwa sababu watakaa sehemu moja na kupata elimu,” amesema.

error: Content is protected !!