November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia awafunda mawaziri, naibu mawaziri, ampangia kazi Lukuvi

Spread the love

 

Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza na mawaziri na naibu mawaziri huku akimpangia kazi aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Rais Samia amezungumza na mawaziri na naibu mawaziri hao leo Alhamisi tarehe 13 Januari, 2022 jijini Dodoma.

Amesema katika masuala ya uratibu wa sekta na wizara mbalimbali, Lukuvi ndiye atamsaidia.

“Kwa hiyo masuala ya uratibu na yenyewe yanahitaji nguvu, na hayo nadhani upande wa waziri mkuu ambao mheshimiwa Lukuvi atakuja kutusaidia kwenye hilo, uratibu wa sekta, wizara mbalimbali na taasisi za serikali,” amesema.

Mbali na kuwapongeza mawaziri hao pia amewapa pole kwa kazi zilizo mbele yao.

Amesema kupitia ilani ya CCM kuna maelekezo wamepewa kuhusu sekta ambapo wanatakiwa kuzingatia kwa lengo ni kutatua shida, dhiki na kuleta huduma bora.

“Pia kuna mpango wa dira wa mwaka 2025 na mpango wa miaka mitano wenyewe umeweka malengo na vipaumbele kadhaa ambavyo sekta zetu tunatakiwa kufanya ili kutoa huduma nzuri na kupiga hatua kimaendeleo kwa nchin yetu

“Sekta tulizozipa kipaumbele ambazo zinamgusa mwananchi moja kwa moja, kama maji, afya, elimu, umeme vijijini.

“Katika kutimiza haya yote kuna suala zima la kufanya kazi kwa pamoja. Kwa wale waliopo kwenye serikali kwa muda mtakumbuka mara kadhaa tumekuwa tukizungumzia masuala ya kufanya kazi kila mtu na lake,” amesema.

Amesema katika wizara nyingi hakuna uratibu ndani ya sekta zenyewe na hata baina ya sekta na sekta.

“Linafanywa jambo moja lakini kila mtu anafanya lake mwisho wa siku unakuja kutafuta outcome ya jambo lililofanywa kila moja anakupa kipande kipande na huliona kwa uzito wake,” amesema.

Aidha, pamoja na hilo Rais Samia amewafunda mawaziri hayo kuhusu mambo mbalimbali tisa ikiwa kutunza siri zetu za serikali, kujenga utamaduni wa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa kazi mbalimbali za serikali na kutatua kero za wananchi na ufuatiliaji wa karibu wa miradi ya Taifa.

Mengine aliyowaonya ni kutoelewana baina yao, kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na ushauri wa watalaam katika utendaji wa kazi, kuwa wabunifu na kutatua changamoto na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea, kufuata taratibu zote katika kuhakikisha watumishi wasiowajibika, wanatimiza tu wajibu na mwisho kutambua kuwa duniani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo moja.

error: Content is protected !!