Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari Rais Samia awaapisha viongozi aliowateua
HabariTangulizi

Rais Samia awaapisha viongozi aliowateua

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua akiwemo Balozi Hussein Kattanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Viongozi hao wakiwemo mawaziri na naibu mawaziri, aliwateua jana Jumatano tarehe 31 Machi 2021.

Viongozi hao, wameapishwa leo Alhamisi tarehe 1 Aprili 2021, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali serikali na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Mawaziri walioapishwa ni, Ummy Mwalimu kuwa Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi; Mohammed Mchengerwa (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) na Seleman Jafo (Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira).

Wengine ni, Prof. Palamagamba Kabudi (Katiba na Sheria), Dk. Mwigulu Nchemba (Fedha na Mipango), Dk. Kitila Mkumbo (Viwanda na Biashara), Goefrey Mwambe (Uwekezaji) na Balozi Liberata Mulamula (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).

Naibu waziri walioapishwa ni, Naibu waziri Ofisi Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, Hamad Hassan Chande, William Tate Olenasha (Uwekezaji), Abdallah Ulega (Mifugo na Uvuvi) na Mwita Waitara (Ujenzi na Uchukuzi).

Pia, Pauline Gekul (Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), Mwanaidi Ally Hamid (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto).

Wengine ni, Mhandisi Hamad Masauni (Fedha na Mipango), Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).

Rais Samia amefanya mabadiliko hayo madogo ya baraza la mawaziri, siku kadhaa tangu alipochukua madaraka ya urais wa Tanzania, kufuatia kifo cha Hayati Dk. John Magufuli, aliyefariki dunia tarehe 17 Machi 2021.

Dk. Magufuli alifariki dunia kwa ugonjwa wa mfumo wa umeme wa moyo, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam, kisha mwili wake ulizikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!