October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia awaapisha RC Shinyanga, Jaji kiongozi, Jaji Mahakama ya rufani

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewaapisha viongozi watatu aliowateua tarehe 8 Oktoba 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Viongozi hao wameapishwa leo Jumatatu, tarehe 11 Oktoba 2021 na Rais Samia, katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Waliopaishwa ni Sofia Mjema, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, akichukua nafasi ya Dk. Philemon Sengati, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Awali, Mjema alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Kiongozi mwingine aliyeapishwa ni, aliyekuwa Jaji wa Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Othman Makungu, kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.

Na, aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, Jaji Mustapha Siyani, kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzaniua.

Jaji Siyani anachukua nafasi ya Jaji Eliezer Feleshi, aliyeteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali hivi karibuni (AG).

error: Content is protected !!