Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia awaapisha majaji 28, Biswalo…
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia awaapisha majaji 28, Biswalo…

Biswalo Mganga (kulia) akiapa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

LICHA ya kelele kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wa upinzani na wanaharakati nchini Tanzania, kupinga uteuzi wa Biswalo Mganga, kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Rais Samia Suluhu Hassan, amemuapisha kushika wadhifa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Biswalo, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), ameapishwa leo Jumatatu, tarehe 17 Mei 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam. Pia, majaji wengine 27 wameapishwa.

Katika kiapo hicho, Jaji Mganga aliapa kutekeleza majukumu yake kwa kufuata misingi ya katiba na sheria za nchi katika kuhakikisha haki inatendekea nchini.

Miongoni mwa waliopiga uteuzi wake ni, Chama Kikuu cha Upinzani nchini humo cha Chadema, ambacho kilimshauri Rais Samia asimwapishe Biswalo, bali aunde Baraza la Nidhamu kwa ajili ya kuchunguza tuhuma dhidi yake.

Chadema kilidai wakati Biswalo akiwa DPP, alitumia madaraka yake vibaya na kusababisha mlundikano wa mahabusu gerezani.

Pia, kilidai kuna uwezekano akawa na mgongano wa kimaslahi kwa sababu mashauri yanaweza kwenda mbele yake kwa rufaa au kuanza kusikilizwa, ambayo alishiriki kuyaandaa.

Mbali na madai ya Chadema, Wakili wa Mahakama Tanzania, Peter Madeleka hivi karibuni alitangaza kumfikisha mahakamani Biswalo kwa madai, alitumia mamlaka yake vibaya alipokuwa DPP, kuweka baadhi ya watu mahabusu, kwa tuhuma za utakatishaji fedha.

Hata hivyo, Biswalo jana Jumapili, alipoulizwa na MwanaHALISI Online juu ya tuhuma hizo hivi karibuni kwa simu, alitaka atafutwe ana kwa ana.

Mbali na Biswalo, Rais Samia pia amewaapisha majaji wa Mahakama ya Rufani saba na wa Mahakama Kuu ya Tanzania 20.

Majaji wa Mahakama ya Rufani walioapishwa ni,

1. Patricia Saleh Fikirini, ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Jaji Mfawidhi – Divisheni ya Biashara, Mahakama Kuu ya Tanzania (Dar es Salaam).
2. Penterine M. Kente ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (Iringa).
3. Dk. Paul Faustine Kihwelo ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama, Lushoto Mkoani Tanga.
4. Lucia Gamuya Kairo ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (Bukoba).
5. Lilian Leonard Mashaka ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Jaji Mfawidhi – Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mahakama Kuu ya Tanzania (Dar es Salaam).
6. Issa John Maige ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Jaji Mfawidhi – Divisheni ya Ardhi, Mahakama Kuu ya Tanzania (Dar es Salaam).
7. Abraham Mwampashi ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Majaji wa Mahakama Kuu walioapishwa ni;

1. Katarina Tengia Revocati ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.
2. Biswalo Eutropius Mganga ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
3. Zahra Abdallah Maruma ambaye kabla ya uteuzi huo, alikuwa Naibu Msajili, Mahakama ya Rufani Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho ya Mahakama (JDU) katika Wizara ya Katiba na Sheria.
4. Devotha C. Kamuzora ambaye kabla ya uteuzi huu, alikuwa Naibu Msajili wa Baraza la Rufani la Kodi (TRAT), Dar es Salaam.
5. Chaba Messe John ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Msajili Mfawidhi, Masjala Kuu ya Mahakama Kuu Dar es Salaam.
6. Lilian Jonas Itemba ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
7. Awamu Ahmada Mbagwa ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ofisi ya Mashtaka Dodoma.
8. Ayoub Yusuf Mwenda ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka.
9. Nyigulile Robert Mwaseba ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania (Dar es Salaam).
10. John Francis Nkwabi ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu (Arusha).
11. Safina Henry Simfukwe ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi.
12. David Patrick Nguyale ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
13. Frank Habibu Mahimbali ambaye kabla uteuzi huu alikuwa Naibu Msajili Mfawidhi, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza.
14. James Karayemaha ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
15. Emmanuel Loitare Ngigwana ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Msajili Baraza la Kodi.
16. Abdi Kagomba ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Meneja wa Huduma za Sheria wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa).
17. Arafa Mpinga Msafiri ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Msaidizi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, Katiba na Sheria, Ofisi ya Rais Ikulu.
18. Dk. Ubena John ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Mhadhiri na Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Mzumbe.
19. Dk. Eliamini Isaya Laltaika ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini.
20. Dk. Theodora Mwenegoha ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
21. Mwanabaraka Saleh Mnyukwa ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Mhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!