Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia awaapisha Ma RAS, Waziri Mkuchika
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia awaapisha Ma RAS, Waziri Mkuchika

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa (RAS) 11 na George Mkuchika, kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais IKulu- Kazi Maalum. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Shughuli hiyo ya kuapishwa, imefanyika leo Jumatano, tarehe 2 Juni 2021, Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma.

Mkuchika, aliteuliwa kuwa waziri kwenye mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri aliyoyafanyia hivi karibuni Rais Samia. Awali, Mkuchika alikuwa waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Ma RAS walioapishwa ni; Rodrick Mpogolo kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi. Kabla ya uteuzi huo, Mpogolo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara na Dk. Athuman Kihamia kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha. Kabla ya uteuzi huo, Dk. Kihamia alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Hassan Abbas Rugwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kabla ya uteuzi huo, Rugwa alikuwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi na Dk. Fatuma Ramadhan Mganga kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Kabla ya uteuzi huo Dk. Mganga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma.

Wengine ni; Mussa Ramadhan Chogello kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huo Chogello alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais na Ngusa Dismas Samike kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Kabla ya uteuzi huo Samike alikuwa Katibu wa Rais, Ikulu wa Hayati Rais John Pombe Magufuli.

Pia, Mhandisi Mwanaisha Tumbo kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Pwani. Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Tumbo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Doroth Aidan Mwaluko kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida. Kabla ya Uteuzi huo, Mwaluko alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) na Balozi Batilda Salha Buriani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga. Kabla ya uteuzi huo, Balozi Buriani aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya na Japan.

Wengine ni; Prisca Joseph Kayombo kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu na Pili Hassan Mnyema kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga. Kabla ya uteuzi huo, Mnyema alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais.

Kabla ya uteuzi huo, Kayombo alikuwa Afisa Mkuu wa Utawala na Utumishi katika Wizara ya Fedha na Mipango

Makatibu Tawala wa Mikoa waliohamishwa vituo vya kazi;

1. Amemhamisha Dk. Seif Abdallah Shekillage aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.
2. Amemhamisha, Karoline Albert Mthapula aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.
3. Amemhamisha, Albert Gabriel Msovela aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.
4. Amemhamisha Dk. Angelina Mageni Lutambi aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya.
5. Amemhamisha, Mariam Amri Mtunguja aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.
6. Amemhamisha, Abdallah Mohamed Malela aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara.
7. Amemhamisha, Judica Haikase Omari aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa Njombe.
8. Amemhamisha, Denis Isdory Bandisa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.
9. Amemhamisha, Missaile Albano Musa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.

Makatibu Tawala wa Mikoa wanaobaki katika vituo vyao vya kazi;

10. Happiness William Seneda anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa.
11. Prof. Faustine Kamuzora anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.
12. Rashid Kassim Mchatta anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma.
13. Rehema Seif Madenge anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi.
14. Steven Mashauri Ndaki anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.
15. Msalika Robert Makungu anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!