May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia auaga mwili wa Mzindakaya, kuzikwa kesho

Rais Samia Suluhu Hassan akiaga mwili wa mwanasiasa mkongwe, Chrisant Majiyatanga Mzindakaya

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameshiriki Ibada ya kumwombea mwanasiasa mkongwe nchini humo, Chrisant Majiyatanga Mzindakaya (80), aliyefariki dunia, Jumatatu ya tarehe 6 Juni 2021, Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwili wa Mzindakaya, umeagzwa leo Jumatano, tarehe 7 Juni 2021, katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay, Dar es Salaam.

Mwili wa Mzindakaya, aliyezaliwa tarehe 31 Desemba 1940, utazikwa kesho Alhamisi, Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mara baada ya shughuli ya kumwombea na kumuaga kumalizika, unasafirishwa kwa ndege mpaka Songwe na kutoka Songwe mwili utapelekwa kwa barabara hadi Sumbawanga.

Enzi za uhai wake, Mzee Mzindakaya amepata kuwa mbunge kwa kipindi cha zaidi ya miaka 40 pamoja na kuhudumu serikalikalini katika nafasi mbalimbali.

error: Content is protected !!