May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia atuma salamu za pole kwa kaka’ke Dk. Mpango, mkewe Shigela

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kwa Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango kufuatia kifo cha kaka yake Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana, Gerald Mpango. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 21 Januari, 2022 na Rais Samia kupitia ukurasa wake wa Twitter, imesema;

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana, Gerald Mpango ambaye ni kaka yake Mhe. Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango. Pole kwa Kanisa, familia, Mhe. Makamu wa Rais, ndugu, jamaa & marafiki. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.

Askofu Mpango amefariki juzi tarehe 19 Januari 2022 Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Enzi za uhai wake Askofu Gerald Mpango alihudumu katika kanisa la Anglikana Dayosisi ya Magharibi ya Tanganyika (Diocese of Western Tanganyika).

Dk Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mazishi ya Askofu Mstaafu Gerald Mpango yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 22 Januari 2022 Kasulu Kigoma ambayo yatatanguliwa na ibada ya kuaga mwili wa marehemu itakayofanyika katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano Posta Dar es salaam leo tarehe 21 Januari 2022.

Katika hatua nyingine Rais Samia pia ametoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shigela kwa kuondokewa na mkewe.

Rais Samia amesema; “Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha mke wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigella, Bi Magdalena Layda.

“Pole kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa, familia, ndugu, jamaa na marafiki. Nawaombea moyo thabiti katika kipindi hiki kigumu. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina”.

error: Content is protected !!