May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia atua Z’bar, kushirki Karume Day

Spread the love

 

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne, tarehe 6 Aprili 2021, amewasili Zanzibar akitokea jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Kesho Jumatano, Rais Samia atahudhuria maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day), itakayofanyika katika Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kisiwandui.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, Rais Samia amepokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.

Baadaye Rais Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

error: Content is protected !!