Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Tangulizi Rais Samia atua nchini, ataja mafanikio ziara Marekani
Tangulizi

Rais Samia atua nchini, ataja mafanikio ziara Marekani

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema ziara yake ya kikazi nchini Marekani, imesaidia kuitangaza Tanzania kwa watu ambao walikuwa hawafahamu rasilimali na fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Kiongozi huyo wa Tanzania, ametaja mafanikio hayo leo Alhamisi, tarehe 28 Aprili 2022, muda mfupi baada ya kuwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), akitokea Marekani alikokuwa kikazi tangu tarehe 13 Aprili mwaka huu.

Rais Samia amesema, amefanikiwa kuitangaza Tanzania, kupitia filamu maalumu iliyotengenezwa kutangaza vivutio vya utalii vya nchi, inayofahamika kwa jina la Tanzania: The Royal Tour.

“Ziara yangu Marekani tumeondoka tukiwa na makusudi ya kwenda kuzindua filamu yetu ya Royal Tour ambayo ina madhumuni ya kujulisha ulimwengu vivutio vilivyoko Tanzania, pia rasilimali tulizo nazo, uwezo na nafasi yetu katika uwekezaji ulimwenguni,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema “ni kweli tumefika, tumeona kwamba kwa nchi moja tuliyokwenda Marekani, bado watu walikuwa hawaijui Tanzania, lakini sasa baada ya ile filamu, tumeacha inaendelea kuchezeshwa katika vituo mbalimbali, sasa watu wataijua Tanzania.”

Rais Samia amesema katika ziara yake Marekani, ujumbe wake ulifanya mazungumzo na uongozi wa Jiji la Dallas na kukubaliana kuanzisha ushirikiano kwenye usafiri wa anga, hivyo kuna uwezekano wa kuwa na ndege zinazotoka moja kwa moja jijini humo , kuja Tanzania.

“Katika ziara yangu kuna kundi lilijimega wakaenda kufanya mkutano kule Dallas na Meya wa jiji hilo, wamekubali na wana hamu tufanye udugu na miji yetu ya Dar es Salaam, Zanzibar, Dodoma na Arusha na miji mingine, wanaangalia uwekezano wa kuwa na ndege za moja kwa moja kutoka Dallas hadi Tanzania kuleta wageni,” amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema taasisi inayofanya utafiti wa wadudu nchini humo (SJRI), imeahidi kuimarisha utendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Taasisi ya Utafiti wa Afya Ifakara na Kituo cha Wadudu Tanga.

Pia, Rais Samia amesema taasisi hiyo imeahidi kujenga vituo vya afya 200 katika mikoa inayoongoza kwa maambukizi ya Malaria.

Aidha, Rais Samia amesema, idadi ya watalii wa kimataifa wanaokuja nchini, imeongezeka kwa asilimia 48.6, baada ya sekta hiyo kuporomoka kutokana na janga lililoikumba dunia la Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19).

“Idadi ya Watalii kimataifa wanaokuja nchini imeongezeka kwa 48.6%, kutoka watalii 620,000 hadi kufikia 922,629. Lakini tunategemea idadi hii itapanda mara mbili. Vilevile, upande wa fedha umeongezeka kutoka Dola 714 Mil (2020), kufikia Dola 1,254 Mil. (2021), hili ni ongezeko la asilimia 76,” amesema Rais Samia.

1 Comment

  • Kuitangaza Tanzania ndio kazi inayofanywa na mkuu wa nchi na amiri jeshi? Mabalozi na mawaziri kazi yao nini?
    Halafu safari hii imegharimu kiasi gani? Wanaojua tafadhali mtupashe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yatoa tamko bungeni sakatala la viboko shuleni

Spread the love  SERIKALI imewaagiza maafisa elimu wa mikoa na wilaya kuratibu...

Habari za SiasaTangulizi

Lema kurejea Machi 3 na sumu ya kuangamiza chawa

Spread the love  HATIMAYE Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia...

error: Content is protected !!