May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia atoa ujumbe wa Pasaka

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewatakia Watanzania wote sikukuu njema ya Pasaka huku akiwakumbusha kuliombda Taifa hilo amani na upendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wakristu wote duniani, leo Jumapili ya tarehe 4 Aprili 2021, wanaadhimisha sikuu ya kufufuka Yesu Kristo.

Rais Samia, ametumia ukurasa wake wa Twitter kutoa salamu hizo za Pasaka akisema “Nawatakia watanzania wote Pasaka njema, tuadhimishe ufufuko wa Yesu Kristo huku tukiliombea Taifa letu la Tanzania kudumisha amani, upendo na mshikamano.”

“Tuendeleze jitihada za kuijenga nchi yetu kwa kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa. Yesu amefufuka, Haleluya Haleluya,” amesema Rais Samia

error: Content is protected !!