December 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia atoa salamu za rambirambi kufuatia ajali ya ndege Bukoba

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania Samia Suluhu ametoa pole kwa wafiwa na majeruhi wa ajali ya ndege iliyotokea Jumapili huko Bukoba, Kagera. Watu 19 walifariki katika ajali hiyo na wengine 26 kuokolewa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika ujumbe wake wa pole, Rais Samia pia amewashukuru wakazi wa Kagera kwa ujasiri, ushirikiano na jitihada walizofanya kuwaokoa abiria waliozama na ndege hiyo.

“Natoa pole kwa familia na wote walioguswa na vifo vya watu 19 waliopoteza maisha katika ajali ya ndege ya Precision iliyotokea Ziwa Victoria. Nawapongeza walioshiriki katika uokozi wakiwemo wananchi wa Bukoba. Nawaombea Marehemu wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka.”

Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kuelekea Bukoba kupitia Mwanza.

Precision Air ndiyo shirika kubwa la ndege la kibinafsi la Tanzania na kwa kiasi fulani inamilikiwa na Kenya Airways. Ilianzishwa mnamo 1993 na inaendesha safari za ndege za ndani na kikanda.

error: Content is protected !!