
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewatakia kheri ya Eid El Fitri Waislamu na Watanzania wote huku akiwataka kusherekea kwa amani na utulivu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Rais Samia ametoa salamu hizo kupitia kurasa zake za kijamii leo Jumanne, tarehe 3 Aprili 2022.
“Kheri ya Eid kwenu nyote. Tusherehekee kwa amani na utulivu huku tukiiombea nchi yetu, tukikumbushana wajibu wa kushiriki katika ujenzi wa Taifa na kuendeleza mafunzo mema tuliyoyapata katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kutoka kwa Mtume wetu Muhammad (SAW). Eid Mubarak,” ameandika Rais Samia.
Kheri ya Eid kwenu nyote. Tusherehekee kwa amani na utulivu huku tukiiombea nchi yetu, tukikumbushana wajibu wa kushiriki katika ujenzi wa Taifa na kuendeleza mafunzo mema tuliyoyapata katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kutoka kwa Mtume wetu Muhammad (SAW).
Eid Mubarak.
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) May 3, 2022
Aidha, mkuu huyo wa nchi, amewaongoza Watanzania katika kushiriki sala ya
Edd El Fitri, kitaifa iliyosaliwa Msikiti wa Mfalme, Muhammad wa Sita wa Morocco, ulioko Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wa kisiasa na kiserikali wamehudhuria sala hiyo akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
More Stories
Uchaguzi TLS: Mtobesya atoa ujumbe
Waziri Mkuu apokea maoni ya wakazi wa Ngorongoro
Ni Profesa Hoseah tena TLS