May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia atoa salamu Eid El Fitri

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewatakoa Watanzania wote sherehe njema ya Eid El Fitri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Leo Ijumaa, tarehe 14 Mei 2021, Waislamu wanasherekea sikuu kuu ya Eid, wakihitimisha mfungo mtukufu wa Ramadhan.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia ametoa salamu hizo akisema “Nawatakia Watanzania wote sherehe njema za Eid El Fitr.”

“Tusherehekee kwa amani na utulivu huku tukiyakumbuka na kuyaenzi mafunzo mema ya Mtume wetu (SAW) na yote tuliyojifunza wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.”

Amemalizia akisema “Mwenyezi Mungu awe nasi daima, Inshaallah. Eid Mubarak.”

error: Content is protected !!