Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia atoa onyo watumishi wa umma, binafsi
Habari Mchanganyiko

Rais Samia atoa onyo watumishi wa umma, binafsi

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka watumishi wa umma na wafanyakazi wa sekta binafsi, kuwa waaminifu kwa kuridhika na vipato halali wanavyopata. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa wito huo leo Ijumaa, tarehe 14 Mei 2021, katika Baraza la Eid El-Fitr, lililofanyika Kitaifa, viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Amewataka wafanyakazi hao kujiupusha na vitendo vya rushwa, wizi na urasimu, kama walivyojiepusha katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani, waendelee vivyo hivyo.

“Nawasihi matendo mema yasiishie jana mwezi ulivyoandama, tuendeleze kufanya matendo mema yenye kumfurahisha Mungu na kuacha mabaya yenye kumchukiza Mungu.”

“Na katika hili, nawasihi sana watumishi wa Serikali na biafsi kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na kupata kipato halali. Wajiepushe na vitendo vya wizi, rushwa, ubadhirifu na urasimu,” amesema Rais Samia.

Pia, kiongozi huyo, amewataka wafanyabiashara nchini, kulipa kodi stahiki kwa ajili ya kuiwezesha Serikali kupata fedha za kuwahudumia wananchi.

“Kwa upande wa wafanyabaishara, nawahimiza kulipa kodi stahiki kwa Serikali, si haki wala uungwana kutolipa kodi. Wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi kutafanya hospitali kukosa dawa na kusababisha vifo, watumishi kukosa mishahara kwa wakati na wanafunzi kukosa elimu bure,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!