Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia atoa mwelekeo mpya Mchuchuma na Liganga
Habari Mchanganyiko

Rais Samia atoa mwelekeo mpya Mchuchuma na Liganga

Spread the love

 

SAMIA Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, ameagiza kuondolewa kwa vikwazo vyote vinavyokwamisha kuanza utekelezaji wa Mradi Unganishi wa Madini ya Chuma na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Liganga, mkoani Njombe. Anaripoti Hamis Mguta, Mwanza …(endelea).

Ni baada ya mradi huo, kutotekelezwa kwa takribani miaka kumi sasa.

Rais Samia ametoa mwelekeo huo mpya, leo Jumapili, tarehe 13 Juni 2021, alipokuwa akizindua Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu, Mkoa wa Mwanza. Ni katika siku ya kwanza kati ya tatu ya ziara yake mkoani humo.

Amesema, uamuzi wa kuondoa vikwazo hivyo ni baada ya kutoendelea kwa kigezo cha kuvutana kati ya Serikali ya Tanzania na mwekezaji ambaye ni Kampuni ya Sichuan Hongda (Group) Company Limited (SHGCL).

Rais Samia amesema, amekwisha kutana na mwekezaji huyo na kufanya naye mazungumzo na kumuahidi kuondoa vikwazo vyote “vya serikali vile ambavyo anaona ni vikwazo ili vibaki kwake sasa kuanza kuchimba.”

“Kisha afuate sheria na lazima afuate sheria na tukimalizana naye huko kwa kufuta vikwazo tuangalie kama anachimba au la,” amesema

Rais Samia amesema, haiwezekani “kila siku tunaweka kwenye mipango, tunaimba mchuchuma na liganga toka mimi nikiwa waziri. Sasa nataka hili lifikie mwisho na tuanze kuchimba sasa na itumike ndani na tuuze nje.”

Tarehe 18 Mei 2021, suala hilo, liliibuka bungeni jijini Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo Mbunge Viti Maalum (CCM), Neema William Mgaya, aliyehoji lini Serikali itaanza utekelezaji wa mradi huo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe alisema, Serikali iliamua kuunda Timu ya Majadiliano kati yake na muwekezaji Kampuni ya Sichuan Hongda (Group) Company Limited (SHGCL), baada ya kampuni hiyo kuomba vivutio ambavyo vinankinzana na baadhi ya Sheria za nchi.

“Ili kuendelea na utekelezaji wa mradi, mwekezaji aliomba vivutio ambavyo vimeshindwa kutolewa na Serikali kwa sababu vinakinzana na baadhi ya Sheria za nchi,” alisema Kigahe.

Alisema “kwa sasa, Serikali ipo katika hatua za uchambuzi wa mradi na kujiridhisha zaidi kuhusu namna bora ya kutekeleza mradi huu, ili kukidhi matakwa ya Sheria mpya Namba 5 na 6 za mwaka 2017 zinazolinda rasilimali za nchi.”

Waziri wa Madini, Doto Biteko

Kigahe alisema mradi huo utaanza kutekelezwa baada ya majadiliano hayo kukamilika.

“Kwa kuzingatia uchambuzi huo, Timu ya Serikali ya Majadiliano ilishaundwa na inaendelea kujadiliana na mwekezaji. Hivyo, utekelezaji wa mradi huu utaendelea mara baada ya kukamilika kwa majadilianobaina ya Serikali na Mwekezaji,” amesema Kigahe.

Alisema baada ya majadiliano hayo kukamilika, mradi huo utatekelezwa kwa ubia kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) yenye hisa asilimia 20 na SHGCL (80%)

“Mradi huu unategemea kutekelezwa kwa ubia kati ya NDC na SHGCL , baada ya majadiliano kuhusiana na baadhi ya vipengele katika mkataba kukamilika,” amesema Kigahe.

Kigahe alisema “Katika utekelezaji wa mradi huu, utafiti wa kina ulikamilika 2012 na kubaini uwepo wa tani milioni 428 za makaa ya mawe katika eneo la Mchuchuma na tani milioni 126 za chuma katika eneo la Liganga.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the loveDEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya Msingi...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the love  DEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya...

error: Content is protected !!