Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia atoa maagizo Tanzania, Uganda
Habari za Siasa

Rais Samia atoa maagizo Tanzania, Uganda

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amezitaka pande zinazoendelea na majadiliano ya ujenzi wa Bomba la Mufuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganga hadi Tanga, Tanzania “kuacha maneno” ili mradi huo ukamilike ifikapo 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia amesema, hayo leo Alhamisi, tarehe 20 Mei 2020, Ikulu ya Dar es Salaam, Tanzania, mara baada ya yeye na Rais wa Uganda, Yoweri Mseven, kushuhudia utiaji saini mikataba ya bomba hilo la mafuta na kampuni za uwekezaji katika mradi huo.

Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa muda wa miaka mitatu (2021 hadi 2024).

Rais Samia amesema, tangu kuanza kwa makubaliano ya ujenzi wa bomba hili, “tumekwisha kusaini mikataba mitano,” nchini Tanzania na mingine Uganda.

Amesema, manufaa ya mradi huu, yapo mengi sana, ajira, matumizi ya korodi, fidia zitakazolipwa na mengi mengi, “mikoa minane na wilaya 24 zitapitiwa na mradi huu na Watanzania tuna deni la kuzalisha ajira milioni saba ndani ya miaka mitano. Mradi huu utatusaida sasna.”

“Nitoe wito kwa pande zote mbili (Tanzania na Uganda), kuhakiklisha tunakamilisha majadiliano ya mikataba iliyobaki ili ikifika mwaka 2025, mafuta yaanze kusafirihswa. Wananchi wetu wamesikia maneno haya kwa miaka mitano nyuma, sasa tuache maneno twende kutekeleza,” amesema Rais Samia

Amesema, kumamilika kwa mradi huo, utaondoa taswira hasi iliyojengeka dhidi ya Bara la Afrika.

“Kwa kipindi kirefu, taswira ya Bara la Afrika, imekuwa na tawira mbaya kama ya vita, njaa na kutokuwa na mazingira bora ya biashara. Kukamilika kwa mradi huu, utachochea mazingira bora ya uwekezaji,” amesema Majaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!