Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari Rais Samia atoa maagizo matatu Tabora
HabariHabari za Siasa

Rais Samia atoa maagizo matatu Tabora

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan, ametoa maagizo matatu kwa wizara na taasisi za Serikali, yenye lengo la kuchochea maendeleo ya wananchi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Maagizo hayo ya Rais Samia yametolewa leo Jumatano tarehe 18, 2022, wakati akizindua barabara ya Tabora-Koga-Mpanda, mkoani Tabora, halfa iliyorushwa mbashara katika vituo vya televisheni mbalimbali nchini.

Katika agizo la kwanza, Rais Samia ameagiza uongozi wa mikoa kuvutia fursa za uwekezaji na kuhamasisha uzalishaji wa wananchi wa mikoa yao.

“Nafahamu hapa Sikonge na ameneo mengine ya Tabora kuna wafugaji wa nyuki, kwa maana hiyo wanazalisha asali. Niwaombe hakikisheni asali inazalishwa kwenye viwango vya kimataifa ili tuweze kufikia masoko ya nje,” amesema Rais Samia.

Agizo la pili lililotolewa na Rais Samia, ni kwa Jeshi la Polisi mkoani Tabora, kuwakamata watu waliohusika na wizi wa miundombinu ya barabara hiyo, ikiwemo taa za barabarani na paneli za sola, uliotokea katika vijiji vinne vya Kasandalala, Tumbili, Usenga na Sikonge Mjini.

“Ni imani yangu kwamba Jeshi la Polisi litawafuatilia wale wote waliohusika na uharibifu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa. Niwaombe sana ndugu zangu tunzeni miundombinu tunayoleta,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amewaoimba wananchi wawafichue watu wanaojihusisha na vitendo vya wizi wa vifaa vya miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara, ili wachukuliwe hatua.

Aidha, Rais Samia ameiagiza Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Taasisi ya Misitu, pamoja na uongozi wa mikoa, kupanga vyema maeneo ya malisho ya wafugaji, ili kuwe na matumizi sahihi ya rasilimali za ardhi.

“Mkiangalia idadi ya watu tulio nao Tanzania, watu wetu wengi ni vijana wadogo ambao wanaendelea kuongeza idadi ya watu. Tutakapotoa maeneo yote ya hifadhi yatumike sana kwa wananchi na vizazi vinayokuja vitakosa maeneo ya kuja kufanya mambo mengine,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewataka wananchi wa Tabora kuongeza nguvu katika uzalishaji wa zao la tumbaku, kwa kuwa soko la uhakika lipo, baada ya muwekezaji kufufua kiwanda cha tumbaku mkoani Morogoro.

1 Comment

  • Asante mama kwa kali njema lakini uwelewe kauli yako bira ufatilliaji kutoka kwakwo ni bure tu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!