May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua wasaidizi wake 9

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Saluhu akihutubia Taifa mara baada ya kuapishwa

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kwenye ofisi yake akiwemo, Juma Selemani Mkomi kuwa katibu wake. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea). 

Uteuzi wa Mkomi umeanza tarehe 19 Machi, 2021.

Taarifa hiyo ya uteuzi, imetolewa jana usiku Ijumaa, tarehe 16 Aprili 2021, na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Pia, Msigwa amesema, Rais Samia amefanya uteuzi wa Wasaidizi katika Ofisi Binafsi ya Rais kama ifuatavyo;

1. Amemteua Said Ali Juma kuwa Mnikulu.

2. Amemteua Balozi Dk. Mussa Julius Lulandala kuwa Msaidizi wa Rais, Nyaraka na Ukalimani (PAP-TD).

3. Amemteua, Balozi Ali Bujiku Sakila kuwa Msaidizi wa Rais, Hotuba (PAP-SD).

4. Amemteua Maulidah Bwanaheri Hassan kuwa Msaidizi wa Rais, Diplomasia (PAP-DA).

5. Amemteua Felister Peter Mdemu kuwa Msaidizi wa Rais, Maendeleo ya Jamii.

6. Amemteua Nehemia Ernest Mandia kuwa Msaidizi wa Rais, Sheria (PAP-LA)

7. Amemteua Blandina Kilama kuwa Msaidizi wa Rais, Uchumi (PAP-EA).

8. Amemteua Dk. Salim Othman kuwa Msaidizi wa Rais, Siasa (PAP-PA).

Msigwa amesema, uteuzi wa Wasaidizi wa Rais umeanza jana Ijumaa.

error: Content is protected !!