May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua viongozi

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwemo, Athumani Mbuttuka kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uteuzi huo umefanywa jana Ijumaa, tarehe 6 Agosti 2021. Teuzi zote zimeanza 5 Agosti, 2021.

Taarifa iliyotolewa na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema, Mbuttuka anachukua nafasi ya Balozi Mohamed Mtonga ambaye amestaafu na Balozi wa Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE).

Kabla ya uteuzi huo, Mbuttuka alikuwa Msajili wa Hazina.

Pia, Rais Samia amemteua Leonard John Mkude kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali. Mkude anachukua nafasi ya Francis Mwakapalila ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Kabla ya uteuzi, Mkude alikuwa Meneja Bajeti, Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Rais Samia amemteua Mgonya Benedict kuwa Msajili wa Hazina. Benedict anachukua nafasi ya Athumani Mbuttuka ambaye ameteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huo, Benedict alikuwa Meneja wa Masuala ya Fedha na Madeni, Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Taarifa imesema, Rais Samia amemteua Frank Mugeta Nyabundege kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo.

Kabla ya uteuzi huo, Nyabundege alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Lake Oil Tanzania Limited.

Pia, amemteua Casmir Kyuki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS. Kyuki ni Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

error: Content is protected !!