May 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua viongozi wawili

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk. Hedwiga Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa, tarehe 23 Aprili 2021 na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, imesema,  Dk. Swai anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Pia, Msigwa amesema, Rais Samia amemteua, Sophia Elias Kaduma kuwa Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS).

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo Ijumaa.

error: Content is protected !!