May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua viongozi wawili

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wawili akiwemo, Profesa Eleuther Alphonce Mwageni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Prof. Mwageni ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) na anachukua nafasi ya Prof. Esther Ishengoma ambaye amemaliza muda wake.

Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema, uteuzi wa Profesa Mwangeni umeanza jana Jumatatu, tarehe 07 Juni, 2021.

Msigwa amesema, Rais Samia amemteua Dk. Neema Bhoke Mwita kuwa Mjumbe wa Baraza la Ushindani (FCC).

Dk. Mwita amechukua nafasi ya Dk. Theodora Nemboyao Mwenegoha ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Uteuzi wa Dk. Mwita umeanza leo Jumanne.

error: Content is protected !!