October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua viongozi watatu

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa wajumbe watatu kujaza nafasi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma …(endelea).

Walioteuliwa ni, Asina Abdillah Omar, ameteuliwa kwa kipindi cha pili kuendelea na majukumu ya Tume.

Ni baada ya kipindi chake cha kwanza kumalizika tarehe 15 Septemba, 2021.

PIli, amemteua Magdalena Kamugisha Rwebangira, kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Tatu, Jaji Jacob Mwambengele, Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Uteuzi huu umeanza tarehe 14 Septemba, 2021.

Taarifa ya uteuzi huo, imetolewa leo Jumatatu, tarehe 27 Septemba 2021 na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

error: Content is protected !!