January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua viongozi 3

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi watatu akiwemo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dk. Baghayo Saqware. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Saqware ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA).

Wengine walioteuliwa ni, Charles Itembe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Eneo Maalum la Mauzi ya Nje (EPZA).

Itembe ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania (Azania Bank Limited).

Aidha, Rais Samia amemteua Ernest Mchanga kuwa Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC). Mchanga ni Katibu Msaidizi, Fedha na Utawala wa JFC kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.

Taarifa ya uteuzi huo, imetolewa leo Jumanne, tarehe 4 Januari 2022 na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu

error: Content is protected !!