October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua viongozi 2

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wawili. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah … (endelea).

Uteuzi huo, umetangazwa leo Alhamisi tarehe 16 Septemba 2021 na Jaffari Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Amewataja walioteuliwa ni Dk. Yamungu Kayandabila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

Dk. Kayandabila ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Pia, Rais Samia amemteua Dk. Naomi Bakunzi Katunzi kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

Uteuzi huo umeanza tarehe 14 Septemba, 2021.

error: Content is protected !!