July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua mrithi wa Mfugale Tanroads

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, amemteua Rogatus Hussein Mativila, kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), akichukua mikoba ya Mhandisi Patrick Mfugale, aliyefariki dunia tarehe 29 Julai 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 30 Julai 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Jaffar Haniu.

Taarifa ya Haniu imesema kuwa, uteuzi huo ulianza tarehe 28 Julai mwaka huu.

“Rais Samia amefanya uteuzi wa viongozi wawili, amemteua Mativila kuwa Mtendaji Mkuu wa Tanroads, anachukua nafasi ya marehemu Mfugale, ambaye alifariki dunia tarehe 29 Juni 2021,” imesema taarifa ya Haniu.

Mativila alikuwa  Mkurugenzi wa Barabara, katika Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi).

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Mfugale alikuwa kiongozi wa Tanroads kwa miaka 10 mfululizo, kuanzia Mei 2011 hadi Juni 2021, alipofariki dunia akiwa hospitalini jijini Dodoma,  baada ya kuugua ghafla.

Mhandisi huyo aliteuliwa kushika wadhifa huo na Hayati Magufuli, alipokuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.

Mbali na uteuzi wa mrithi wa Mfugale, Rais Samia amemteua Prof. Yunus Mgaya, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Mgaya alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

error: Content is protected !!