Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan leo tarehe 8 Januari, 2022 amefanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri na nafasi za makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu huku akiteua mawaziri wapya watano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika taarifa iliyosomwa kwa umma kupitia vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga, Nape Nnauye ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Aliyekuwa Naibu Waziri Fedha na Mipango, Hamadi Yusuph Masauni ameteuliwa kuwa waziri wizara ya mambo ya ndani ya nchi.

Dk. Pindi Chana ameteuliwa kuwa Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu atakayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratitbu.

Rais Samia pia amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula kuwa waziri wa wizara hiyo.

Wakati aliyekuwa naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe amemteua kuwa waziri wa kilimo.

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *