May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua makatibu wakuu, Msigwa wa Ikulu…

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wakiwemo makatibu wakuu na wakuu wa taasisi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uteuzi huo umefannyika leo Jumapili tarehe 4 Aprili 2021 na kutangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa.

Miongoni mwa walioteuliwa ni Gerson Msigwa ambaye ameteuliwa kuwa, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Pia, amemteua Jabir Bakari Kuwe, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA). Anachukua nafasi ya James Kilaba.

Soma uteuzi wote alioufanya Rais Samia ambapo watele wataapishwa Jumanne tarehe 6 Aprili 2021, Ikulu ya Dar es Salaam.

error: Content is protected !!