May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua mabalozi 23 akiwemo Hoyce Temu

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa mabalozi 23, akiwemo Hoyce Anderson Temu, ambaye ni mwandishi wa habari na mjasiriamali. Anaripoti Matilda Peter, Dar es Salaam…(endelea).

Pia, Temu amewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1999.

Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imesema, uteuzi wa mabalozi hao umeanza leo Jumamosi, tarehe 22 Mei, 2021 na wataapishwa kwa tarehe zitakazotangazwa baadaye.

Uteuzi huu wa mabalozi 23, ni ishara kuwa watakwenda kuchukua nafasi ya mabalozi watakaostaafu, kujaza nafasi za balozi zilizo wazi na wengine kupangiwa kazi zingine.

Hoyce Temu

Mabalozi hao walioteuliwa ni;

1. Amemteua Lut. Jen. Yakub Hassan Mohamed. Lut. Jen. Yakub ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
2. Amemteua Mej. Jen. Richard Mutayoba Makanzo. Mej. Jen. Makanzo ni Mkuu wa Kamandi ya Wanamaji ya JWTZ.
3. Amemteua Bw. Pereira Ame Silima. Bw. Silima ni Naibu Waziri Mstaafu wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
4. Amemteua Bi. Maulidah Bwanaheri Hassan. Bi. Maulidah ni Msaidizi wa Rais Diplomasia, Ofisi ya Rais Ikulu.
5. Amemteua Bw. Togolani Edriss Mavura. Bw. Mavura ni Msaidizi wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
6. Amemteua Bw. Edwin Novath Rutegaruka. Bw. Rutegaruka ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).
7. Amemteua Bw. Fredrick Ibrahim Kibuta. Bw. Kibuta ni Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu.
8. Amemteua Bw. Noel Emmanuel Kaganda. Bw. Kaganda ni Afisa Medani, Ofisi ya Rais, Ikulu.
9. Amemteua Bi. Mindi H. Kasiga. Bi. Mindi ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
10. Amemteua Bi. Caroline Kitana Chipeta. Bi. Chipeta ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
11. Amemteua Bw. Macocha Moshe Tembele. Bw. Tembele ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
12. Amemteua Bi. Agnes Richard Kayola. Bi. Kayola ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
13. Amemteua Bw. Masoud Abdallah Balozi. Bw. Balozi ni Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje – Zanzibar, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
14. Amemteua Bw. Ceasar George Waitara. Bw. Waitara ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
15. Amemteua Bi. Swahiba Habib Mndeme. Bi. Mndeme ni Afisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania Washington D.C nchini Marekani.
16. Amemteua Bw. Said Juma Mshana. Bw. Mshana ni Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu.
17. Amemteua Bw. Alex Gabriel Kallua. Bw. Kallua ni Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu
18. Amemteua Bw. Mahmoud Thabit Kombo. Bw. Kombo ni Waziri Mstaafu wa Utalii na Mambo ya Kale, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Zanzibar.
19. Amemteua Bw. James Gillawa Bwana. Bw. Bwana ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Shinyanga.
20. Amemteua Bi. Hoyce Anderson Temu. Bi. Temu ni Mwandishi wa Habari na Mjasiriamali.
21. Amemteua Bw. Said Shaib Mussa. Bw. Said ni Naibu Mkurugenzi, Ofisi ya Rais, Zanzibar.
22. Amemteua Bi. Elsie Sia Kanza. Bi. Kanza ni Mshauri Maalum wa Rais kwenye Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum).
23. Amemteua Bw. Robert Kainula Kahendaguza. Bw. Kahendaguza ni Naibu Balozi, Umoja wa Mataifa, Geneva.

error: Content is protected !!